Mara nyingi nimetokea kupenda kile ninachokiita mabadiliko ya kisiasa Tanzania,kwa sababu mabadiliko hayo yatamsaidia Mtanzania mnyonge kwa sauti yake kusikika. Ni miaka takribani 19 toka mwaka 19991 uliporuhusiwa mfumo wa vyama vingi. Wakati asilimia 20 ilikubali kuanzishwa kwa vyama vingi asilimia 80 ilipinga suala hilo,hayo ni kwa mujibu wa matokea ya Tume ya Jaji Nyalali.Lakini kwa kuendana na mabadiliko ya dunia ,Serikali kwa wakati huo chini ya Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi iliamua kwa moyo mmoja kuruhusu mfumo wa vyama vingi nakumbuka Rais Mwinyi maarufu kama Mzee Ruksa aliwahi kudokezea kuwa kutakuja utitiri wa vyama lakini hivyo vyote vitajichuja vyenyewe kutokana na sera zao kwa wananchi nakuita utitiri huo wa vyama kuwa ni "riziki dudu" kwani kuwepo kwake kuna watakopata kula humo humo.
Nikija kwenye mada yangu nina wasiwasi na baadhi ya wanasiasa kwa kutupa wakati mgumu hasa linapokuja suala la kiongozi wa chama kuhama chama kimoja kwenda chengine na huku nyuma akitoa kashfa nzito za kwanini amehama na wakati huo huo mwengine anatoka chama hicho na kuhamia chengine na kutoa kashfa kama hizo.Ni haki ya kiraia kuamua kuwa mfuasi wa chama unachokipenda lakini haingii akilini kuwa ni mtu makini unapokuwa ni mtu wa kuhama hama.
Hivi karibuni, baada ya Uchaguzi mkuu na kwa mara ya kwanza vyama vya upinzani hasa Chadema kupata viti vingi bungeni kwa kweli ni jambo la kujifahari. Ila nina patwa na wasi wasi kwanini kuna malalamiko kwa baadhi ya viongozi waliokuwa wa Chadema kulalamikia Uongozi Mkuu unawatupa mkono linapokuja suala la kuwasaidia wakati wanapokabiliwa na matatizo. Wiki hii Mwenyekii wa Chadema mkoa wa Mbeya Bwana Sambwee Shitabala ametangaza kujiuzulu ili kupisha uchunguzi ufanyike wa madai ya kupokea mlungula wa milioni 600 ili kukihujumu chama."Nimeamua kuachia ngazi kwa hiari yangu, nimetuhumiwa kuhujumu chama. Nimeambiwa nimehongwa mamilioni ya fedha na CCM ili nikikoseshe ushindi chama changu, naachia ngazi ili uchunguzi dhidi ya tuhuma hizi ufanyike," alisema Bw. Shitambala. Aliendelea kwa kusema inaonesha chuki hii imepandwa kwa wanachama wa ngazi ya mkoa hadi Taifa nakutoatela mfano wa mwenyekiti wake Bwana Freeman Mbowe kutpokea simu yake"Inaonesha mbegu hii imepandwa na kukubalika kwa wanachama….nimempigia simu mwenyekiti wangu wa Taifa mara kadhaa lakini hapokei simu yangu, hili si jambo la kawaida, bora niachie ngazi," alisisitiza Bw. Shitambala.
Tukiachana na huyo leo hii Mwenyekiti wa baraza la wanawake Chadema Bi Leticia Ghati Mosore ametangaza kujiuzulu kwa kile anachodai kutotahaminiwa cheo chake.Akizungumza na waandishi wa habari waliofika leo katika makao makuu ya chama cha NCCR-Mageuzi kumsikiliza akitangaza nia yake ya kukihama chama cha CHADEMA na kujiunga na NCCR-Mageuzi kwa madai kwamba amechoshwa na taratibu nzima za uongozi wa juu wa chama hicho na kutopewa umuhimu wa cheo chake katika shughuli mbali mbali za kichama zikiwemo za baraza la wanawake ambalo yeye ndio mwenyekiti wake.
Hivyo basi ningeomba kwa uongozi mkuu wa Chadema kujiangalia tena kabla ya kushutumu kuwa kina hujumiwa kwani badala ya kujijenga na kuwa imara kisije tokea kama yale yaliyosababisha kusambaratika kwa chama kama NCCR-Mageuzi.Hakuna adui anaefurahia adui wake kufanikiwa lakini kabla huja toka nje hebu tizama ndani kwako au wewe mwenyewe kuwa hakuna makosa yatakayopelekea adui yako kutumia mwanya huo kukusambaratisha.
Video hapo chini inaonesha mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Muheza alipojiunga na CCM,JE! Uongozi wa Chadema kuna nini nyuma ya pazia?.
Mtazamohalisi
Tuesday, November 23, 2010
Monday, November 22, 2010
Tarik Aziz Ahaha Kutaka Msamaha wa Rais wa Iraq
| Toka shoto ni Tarik Aziz akiwa na Saddam Hussein wakati wa utawala wao |
Mawakili wa Tarik Aziz wamuomba Rais wa Iraqkumsamehe mshirika wa Saddam Hussein,aliyehukumiwa kunyongwa kwa mauaji ya mashia.
Aziz alikuwa mwakilishi wa kimataifa katika utawala wa Saddam Hussein na mkristo pekee katika baraza la mawaziri akiwa anashikilia vyeo vya waziri wa mambo ya nje na naibu waziri mkuu.
Wakili wake,Giovanni Di Stefano,amesema ana matarajio ya mteja wake kupata msamaha, kutokana na kuombewa msamaha na mataifa ya ulaya na Vatican, na pia kitendo cha rais wa Iraq Jalal Talabani kukataa kuweka sahihi ya kuruhusu kunyLakini kuna utata kama Talabani anaweza kumsamehe Aziz,kwani msamaha wa rais kwa mujibu wa katiba ya Iraq lazima kupata ridhaa ya waziri mkuu ambaye ni shia.
Chanzo: http://gulfnews.com/news/region/iraq/tarek-aziz-seeks-pardon-from-iraqi-president-1.716113
Urusi Ya Laani Bwana Bout(Merchant Of Death) Kupelekwa Amerika
Baraza la mawaziri la Thailand limefikia muafaka wa kumpeleka uhamishoni nchini Amerika ,mfanyabiashara wa silaha raia wa Urusi Bwana Victor Bout maarufu kama Merchant of Death baada ya mvutano wa kisheria wa muda mrefu wa ama kumsimamisha kujibu mashtaka au kumuachia huru.
Bwana Victor Bout ,43 afisa wa zamani katika jeshi la anga la urusi alikamatwa Hotelini mjini Bangkok mnamo mwezi march 2008 kwa ushirikiano wa maafisa wa usalama wa Thailand na Mawakala wa ujasusi toka Amerika.
Anashutumiwa kusambaza silaha zilizo chochea vita ya kiraia katika nchi za kusini mwa Amerika,Mashariki ya Kati na Afrika miongoni mwa wateja wake ni Rais wa zamani wa Liberia Charles Taylor,na kiongozi wa Libya Muumar Gadhafi- na pia Angola pande zote mbili(MPLA na UNITA) .
Kitendo hicho cha uhamisho wake toka Thailand kwenda Amerika kumeibua vita ya kidiplomasia baina ya Urusi na Amerika.Wakati serikali ya Amerika imefurahia kumpata Bwana Bout ambaye yupo katika orodha ya watu hatari duniani,Urusi wamelaani kitendo hicho nakusema haki haikutendeka kwani Bwana Bout ni mtu safi.
Baada ya hilo tukio hebu angalia movie hii utajua ni hatari gani ya wafanyabiashara wa silaha wasivyojali watu maskini hasa Afrika. Angalia trailer kisha click link hapo chini uangalie full movie.
LORD OF WAR BY NICOLAS CAGE
Na hii link ni vipande vya filamu nzima: http://www.youtube.com/watch?v=1KGu0FMDJfk&feature=related
| Bwana Victor Bout akiwa chini ya ulinzi nchini Thailand |

Kesi Ya Uhalifu Wa Vita Dhidi ya Bemba ni Jumatatu Hii
Kiongozi wa chama cha upinzani MLC, Jean-Pierre Bemba akipiga kura Kinshasa, DRC 2006.
"Jean-Pierre Bemba atafikishwa mahakamani Jumatatu, Novemba 22, kwa mashtaka ya uhalifu wa vita na uhalifu dhidi ya ubinadamu ulotendwa CAR kati ya 2002 na 2003." amesema bi Daphne Anayiotos
Kesi ya uhalifu wa vita dhidi ya makamu rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jean Pierre Bemba, inanaza The Hague, Uholanzi Jumatatu kufuatana na Mahkama ya Uhalifu wa Kimataifa, ICC.Msemaji wa ICC Daphne Anayiotos, ameiambia Sauti Ya Amerika kwamba Bermba anashtakiwa kwa tuhuma za uhalifu ulotendwa na wapiganaji wake huko Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Bi Anayiotos amesema, "Jean-Pierre Bemba atafikishwa mahakamani Jumatatu, Novemba 22, kwa mashtaka ya uhalifu wa vita na uhalifu dhidi ya ubinadamu ulotendwa CAR kati ya 2002 na 2003."
Serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, iliwasilisha mashtaka hayo mbele ya ICC 2004. Wakosowaji wanashuku na mashtaka hayo wakidai kwamba Rais Ange-Felix Patasse ndiye aliyemualika Bembe kumsaidia kuzima uwasi nchini mwake.
Chanzo:Voa swahili
Rais wa Comoro Amtembelea JK Ikulu Leo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Ikulu jijini Dar es Salaam ,
Rais wa Muungano wa Visiwa vya Comoro Ahmed Abdallah Mohamed
Sambi leo mchana.Viongozi hao wawili baadaye walifanya mazungumzo
(picha na Freddy Maro)
Sunday, November 21, 2010
Wafurahia Papa Kuruhusu Kondomu
Wapenda mabadiliko katika Kanisa Katoliki na makundi ya kupambana na UKIMWI yamefurahia matamshi ya Papa Benedikt kuwa matumizi ya kondomu sio mara zote ni ya nia mbaya.
Ruksa... Ingawa katika mazingira fulani tu.
Papa amesema matumizi ya mipira hiyo ya kiume inaweza kuhalalishwa kutokana na hali ilivyo, ili kuzuia kusambaa kwa maambukizi ya virusi vya HIV/UKIMWI.
Matamshi hayo yanayotarajiwa kuchapishwa katika kitabu wiki ijayo, yanaashiria kulegeza msimamo wake mkali wa zamani dhidi ya matumizi wa kondomu kupambana na HIV.
Vatikana kwa muda mrefu imekuwa ikipinga matumizi ya kondomu, kama njia ya kupanga uzazi.
Wanaharakati wamefurahishwa na uamuzi wa Papa
Hatua hiyo ilizua shutuma kali, hasa kutoka kwa wanaharakati wa kupambana na UKIMWI, ambao wanasema kondomu ni moja ya njia ambazo zimethibitishwa katika kupambana na maambukizi ya HIV.
Papa Benedikt katika ziara yake nchini Cameroon mwaka jana alisema kugawa kondomu kunaweza kuchochea maambukizi ya HIV, matamshi ambayo yalizua shutuma kutoka kwa nchi kadhaa za Umoja wa Ulaya.
Hata hivyo, katika matamshi yake ya hivi karibuni, amesema matumizi wa kondomu yanaweza kuhalalishwa katika mazingira fulani ya kipekee.
Ametoa mfano wa makahaba wa kiume, ambapo amesema matumizi wa kondomu kuzuia maambukizi ya UKIMWI yanaweza kuonekana kama kitendo cha mtu kuwa na majumuku, ingawa amesema kondomu "sio njia halisi ya kupambana na uovu wa kuambukiwa HIV".
Chanzo: BBC
50 Cent anakuja na kali"Things Fall Apart"
Sanaa ni kazi hasa pale unapotakiwa kuivaa tabia halisi ya kile unachoigiza, na kazi kubwa ni kuwa tayari kwa gharama yoyote hata iwe kujibadilisha muonekano na hadhi yako.
Mathalani tumeshuhudia mara nyingi kwa kuona waigizaji kama Will Smith alivyofanikiwa kuigiza kama Mohamed Ali na Beyonce kupunguza uzito kwa pauni 20 kwa siku 10.
Lakini wote hao tisa, kumi ni curtis"50 cent" Jackson mwenye uzito wa pauni 214 alipojipunguza kwa pauni 54 ili kufikia lengo la pauni 160 kwa ajili ya filamu yake mpya "Things Fall Apart". Kwa muda wa wiki 9 amekuwa katika mlo maalumu ili kuuvaa uhalisi wa mchezaji wa American Football ambaye aliugua ugonjwa wa kansa.
Hebu angalia picha alizotoa wakati akiitangaza filamu hiyo mpya, kisha ujiulize kama itawezekana kwa msanii wa bongo kuweza kuigiza mathalani hata sehemu ya harakati za Mwalimu Nyerere.

Katika picha ya kwanza na ya pili ndivyo atakavyoonekana katika filamu hiyo.
Na picha ya tatu jinsi 50 cent akiwa katika muonekano halisi.
Kazi kwenu wasanii, ujumbe umefika .

Subscribe to:
Posts (Atom)