Mtazamohalisi

Friday, January 28, 2011

Mganda Atumia Kigezo cha Ushoga Kudai Haki Ya Ukimbizi

Hatua kali ya sheria ya ushoga nchini Uganda kumempelekea Brenda Namigadde,mwanamama wa kiganda kuiomba serikali ya Uingereza kumfikiria kupata haki ya ukimbizi kuliko kurudishwa nchini Uganda.

Kwa mujibu wa mwanamama huyo ambaye amedai ni Msagaji na kwamba ni uvunjaji wa sheria nchini kwake kuwa na uhusiano wa jinsia moja hivyo kurejeshwa kwake kutahatarisha maisha yake.

Kwa mujibu wa sheria ya Uganda, ni marufuku kuwa na uhusiano wa mapenzi na mtu wa jinsia moja na yeyote atakae vunja sheria hukumu yake ni miaka 14 licha ya juhudi kubwa kugonga ukuta kwa baadhi ya wabunge waliofika mbali nakutaka "hukumu ya kifo" itumike.

Wiki hii nchini Uganda imeshuhudia mtetezi mkuu wa haki za mashoga David Kato  akiuawa na mtu asiyejulikana mara baada ya kuvamiwa nyumbani kwake,nakifo chake kimeibua hisia za watetezi wa haki za binadamu na wapenzi wa haki za mashoga kuhofia usalama wao.

Kwa mujibu wa hukumu ya Bi.Brenda Namigadde, wizara ya mambo ya ndani imeshindwa kujiridhisha na ushahidi alioutoa kwa kuwa hana vidhibitisho kuwa yeye ni Msagaji.Hivyo madai yake batili.

Hata hivyo Bi Breanda Namigadde amekata rufaa na kupeleka vielelezo zaidi ili kuiridhisha idara ya mambo yandani ya Uingereza ambayo imevipokea na kuanza kuvipitia.

Ikiwa ushahidi hautotesheleza vigezo kwa mujibu wa sheria ya Uingereza ,basi muhusika itampasa kufunga virago.

Umoja wa mataifa kupitia kamishna wake wa masuala ya wakimbizi Bw.Antonio Guterres amenukuliwa akizitaka mamlaka za kimataifa kuwapokea wakimbizi toka Uganda waliokimbia kutokana na maisha yao kuwa hatarini.
Chanzo:  BBC

Video ya David Kato kabla na baada ya Mauaji yake

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...