Mifugo ikitaabika kutokana na ukame ulosabibisha kukosa lishe
na maji.
Utafiti uliofanyika toka Discover Magazine umegundua ya kuwa kutokana na tatizo la chakula duniani,ukame wa ardhi,maji na uharibifu wa mazingira ili kuokoa mazingira hatua mbadala zinapaswa kuchukuliwa ikiwamo kubadili aina ya maakuli yetu.
Utafiti umegundua ya kuwa ufugaji wa wadudu kama senene,kumbi kumbi,barare na aina za minyoo hauhitaji mradi mkubwa wa ardhi,maji, kwani upatikanaji wake hauhitaji uangalizi mkubwa kama ule wa mifugo ya ng'ombe,mbuzi ,kondoo,nguruwe ambao wanahitaji ardhi na maji ya kutosha hali inayopelekea uhaba wa ardhi na maji hivyo kusababisha ukame na uhaba wa chakula.
Ripoti ya umoja mataifa ya mwaka 2006 inasema kuwa sekta ya ufugaji huchangia 18% ya uchafuzi wa mazingira duniani kwa kuzalisha kaboni kuliko sekta ya usafirishaji na ndio chanzo kikuu cha kusababisha ukame wa ardhi na maji.Katika utafiti huo wametahadharisha ya kuwa ifikapo mwaka 2050 uzalisha wa wanyama hao utafikia tani 465 maradufu ya takwimu ya mwaka 2000.
Katika toleo hilo umemalizia kwa kuelezea ya kuwa wadudu wanakiasi kidogo cha protini na mlo mzuri kuliko nyama kwani wanyama wana mafuta mengi ambayo ni hatari kwa afya.
No comments:
Post a Comment