Mtazamohalisi

Sunday, December 26, 2010

JK AMTEUA MOHAMED CHANDE OTHMAN KUWA JAJI MKUU MPYA

                                                                                                      

                                    UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
                      DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
                                  Telephone: 255-22-2114512, 2116539
                                       E-mail: press@ikulu.go.tz
                                  Website: www.mawasilianoikulu.go.tz
                                       Fax: 255-22-2113425


                                       PRESIDENT’S OFFICE,
                                       THE STATE HOUSE,
                                        P.O. BOX 9120,
                                        DAR ES SALAAM.
                                        Tanzania.


                           TAARIFA YA IKULU
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Jaji Mohamed Chande Othman kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania, kuanzia tarehe 28 Disemba, 2010.

Jaji Othman anachukua nafasi ya Jaji Augustino Ramadhani anayestaafu kwa mujibu wa sheria tarehe 27 Disemba, 2010.

Jaji Othman amekuwa Jaji wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa kwa muda miaka saba(7).

Kwa sasa Jaji Othman ni Jaji wa Mahakama ya Rufaa na pia ni mtaalamu binafsi juu ya hali ya Haki za Binadamu huko Kusini mwa Sudan, hadi mwezi Agosti 2011.

Jaji Othman alizaliwa tarehe 1 Januari, 1952, ana shahada ya kwanza ya Sheria (LLB) ya Chuo Kikuu cha Dar-Es-Salaam na Shahada ya Uzamili (MA) kutoka katika Chuo Kikuu cha Webster, Geneva-Uswisi.

Amewahi kuwa Makamu wa Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Rwanda huko Arusha na amewahi kushika nafasi sawa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali huko Timor Mashariki.

Jaji Othman pia, amewahi kufanya kazi ndani na nje ya nchi katika Mashirika mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa kama vile Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP) na Shirika la Msalaba Mwekundu.

Jaji Othman ataapishwa kesho tarehe 27 Disemba, 2010 katika viwanja vya Ikulu saa 4:00 asubuhi.

                                      Michael P. Mwanda,
                                      Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi,
                                                 Ikulu.
                                          DAR ES SALAAM.
                                          26 Disemba, 2010

Saturday, December 25, 2010

Nazi Zao Yatima Hana Mzazi Hana Mlezi


Zao la Mnazi kwa biashara tukiamua tunaweza.

Nikianza kwa kunukuu maneno ya Rais Kikwete kuwa zao la minazi limepatwa na " Ugojwa usiotibika kwa sasa ",nakuwataka wakulima wa zao la mnazi kulima kokoa kama zao mbadala .Wazo kama hili si geni ,kwani hapo nyuma wakulima huko Mwanza walitakiwa kubadilisha zao la pamba kwa kahawa .

Inaniwia vigumu kukubaliana na Rais hasa pale alipowahakikishia wakulima wa zao la  minazi kuwa atawapa wataalamu kushirikiana nao ili kuweza kufanikisha zoezi hili la kubadilisha Mnazi kwa Kokoa, na ndiyo hapo sera ya kilimo kwanza ninapohisi kushindwa.

Lengo kuu la kilimo kwanza ni kumkomboa mkulima mdogo toka kilimo cha kuchumia tumbo hadi kilimo chenye kunyanyua kipato cha mkulima na serikali . Na ndipo hapo ninakuwa na shaka na mkulima wa minazi kumuona kuwa ni yatima hana mzazi wala mlezi.

Minazi mingi iliyopo imetokana na mashamba ya kurithi ambayo huenda tumerithi toka kwa wazee wetu ama mara baada ya harakati za ukombozi wananchi kujimilikisha kama matunda ya uhuru.

Kutokana na umri mrefu na kutoboreshwa mashamba kutokana na uwezo duni au tamaa za wenye mashamba kwa kuangalia mavuno bila kutahadhari uboreshwaji wa zao hilo kwa kukuza miche mipya na uwekaji wa mbolea , zao hili limejikuta siku hadi siku likiwa linatokomea.

Miaka ya 80 hadi 90 zao hili lilikuwa likishughulikiwa na Mradi wa Kitaifa wa Kuendeleza Zao la Mnazi , vipi iwezekane kutoa wataalamu kuwezesha kubadilishwa zao moja kwenda lengine na kusiwezekane kutoa wataalamu wa kuendeleza na kuboresha zao lililopo.

Ushauri wangu kwa wizara husika hasa ya kilimo na mazingira,jaribuni kufanya utafiti kujua jinsi gani ya kuokoa utowekaji wa zao la mnazi na pia ili serikali ijiridhishe haina budi kuchukua uzoefu wa nchi nyengine mfano wa  Sri lanka , kwani kisiwa hichi kinafaidika sana na zao la Mnazi.

Ukitazama athari iliyopo ni kuwa,zao la mnazi likiboreshwa litanyanyua kiwango cha maisha kwani nazi hutumika sana kwa mapishi,kutoa mafuta na ni kiburudisho cha koo na uboreshwaji wake utanyanyua uchumi kwa nchi na wananchi .

Zao la Mnazi ni alama kuu katika ukanda wa pwani ya Afrika Mashariki na ukiangalia kwa makini  kutokomea kwake ni sawa na kuondoa meno halisi na kuyabadili kwa meno bandia.Kutokana na umri mrefu na kutoboreshwa mashamba kutokana na uwezo duni au tamaa za wenye mashamba kwa kuangalia mavuno bila kutahadhari uboreshwaji wa zao hilo kwa kukuza miche mipya na uwekaji wa mbolea , zao hili limejikuta siku hadi siku likiwa linatokomea.

Miaka ya 80 hadi 90 zao hili lilikuwa likishughulikiwa na Mradi wa Kitaifa wa Kuendeleza Zao la Mnazi , vipi iwezekane kutoa wataalamu kuwezesha kubadilishwa zao moja kwenda lengine na kusiwezekane kutoa wataalamu wa kuendeleza na kuboresha zao lililopo.

Ushauri wangu kwa wizara husika hasa ya kilimo na mazingira,jaribuni kufanya utafiti kujua jinsi gani ya kuokoa utowekaji wa zao la mnazi na pia ili serikali ijiridhishe haina budi kuchukua uzoefu wa nchi nyengine mfano wa  Sri lanka, kwani kisiwa hichi kinafaidika sana na zao la Mnazi.

Ukitazama athari iliyopo ni kuwa,zao la mnazi likiboreshwa litanyanyua kiwango cha maisha kwani nazi hutumika sana kwa mapishi,kutoa mafuta na ni kiburudisho cha koo na uboreshwaji wake utanyanyua uchumi kwa nchi na wananchi .

Zao la Mnazi ni alama kuu katika ukanda wa pwani ya Afrika Mashariki na ukiangalia kwa makini kutokomea kwake ni sawa na kuondoa meno halisi na kuyabadili kwa meno ya bandia.

Majembe yaondolewa barabarani

Serikali imeiagiza Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), kuvunja mkataba na Kampuni ya Udalali ya Majembe Auction Mart ya jijini Dar es Salaam Desemba 31, mwaka huu.

Majembe ilipewa na Sumatra mkataba wa uwakala wa kusimamia shughuli za daladala jijini Dar es Salaam kwa miaka miwili kuanzia mapema mwaka huu.

Akizungumza na Waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Waziri wa Uchukuzi, Omar Nundu, alisema kuvunjwa kwa mkataba huo kutasaidia kupunguza kero zinazosababishwa na Majembe.

Nundu alisema wameamua kuuvunja mkataba huo kutokana na Majembe kuendelea kukiuka sheria na kanuni walizopewa wakati wa kabla ya kuanza kufanya kazi za uwakala.

Kwa Mujibu wa Waziri huyo, Majembe ilianza kufanya kazi ambazo haziwahusu na ambazo hawana ujuzi nazo, ikiwa ni pamoja na zile za usalama barabarani.

Alisema zipo baadhi ya kazi zinazotakiwa kufanya na askari wa kikosi cha usalama barabarani, lakini kinyume chake zimekuwa zikifanywa na Majembe, jambo ambalo ni kuingilia kazi zisizowahusu.

" Hii siyo sawa, hatutakiwi kuweka watu watufanyie kazi wasizo na uzoefu nazo…lazima tuweke mfumo madhubuti utakaotusaidia kutatua matatizo, si kuweka weka tu, watu wasio na utaalamu," alisisitiza.

Alisema baadhi ya kazi ambazo ni kinyume na sheria zinazofanywa na Majembe ni pamoja na kukagua magurudumu ya magari, leseni, bima, taa za magari na vioo.

Waziri huyo alisema ikiwa Sumatra watahitaji kuendelea kufanya kazi na Majembe, wanatakiwa wawape mafunzo maofisa wake kwanza kuhusu namna kufuata sheria za usalama barabarani.

Sumatra iliipa Kampuni hiyo mkataba huo kwa lengo la kuboresha usafiri wa umma na kuondoa kero kwa wakazi wa Dar es Salaam, kusimamia, kufuatia na kufanya ukaguzi wa utekelezaji wa masharti ya leseni.

Kabla Majembe haijapewa mkataba huo, wakazi wa Dar es Salaam walikuwa wakilalamikia vitendo vya ukiukwaji wa sheria vilivyokuwa vikifanywa na daladala kama kukatisha safari, kushusha na kupakia abiria katika maeneo yasiyo na vituo, makondakta na madereva kutovaa sare, kutoza nauli za juu, matusi na kukataa kuwabeba wanafunzi.

Moja ya sababu ambazo hivi karibuni zilikuwa zikilalamikiwa na wamiliki wa mabasi ya mikoani na daladala dhidi ya Sumatra ni kuiruhusu Majembe kuweka wafanyakazi kufanya kazi za barabarani.

Mapema mwezi huu, wamiliki wa mabasi walitishia kugoma pamoja na mambo mengine, wakitaka kampuni hiyo isijihusishe na kazi za barabarani bila kuwepo na askari wa kikosi cha usalama barabarani..

Wakati huo huo; Serikali imetangaza kuwaondoa mara moja wapiga debe katika vituo vyote vya mabasi nchini.

Nundu alizitaka mamlaka zinazohusika kuandaa utaratibu wa kuwatambua wafanyakazi na mawakala wa makampuni ya mabasi kwa kuwapatia vitambulisho maalum.

Alisema utaratibu wa kuhakikisha wapiga debe wanaondoka katika vituo vya mabasi unatakiwa kufanyika sasa na kwamba ifikapo Januari 15, mwakani, utaratibu wa kutoa vitamburisho kwa wafanyakazi na mawakala unatakiwa uwe umekamilika.

" Ninaagiza kwamba kuanzia sasa ninataka kuona wapiga debe wote wameondolewa katika vituo vyote vya mabasi, na zoezi hili linatakiwa kufanyika haraka iwezekanavyo,” alisema.

Aliongeza kuwa wapigadebe wamekuwa kero kubwa kwa wasafiri hususani wa mikoani kusumbuliwa wanapokwenda kukata tiketi na wakati mwingine kuwaibia.

Kwa upande mwingine, Nundu alisema kuna umuhimu wa kuwepo kwa matuta barabarani ili kupunguza ajali zinazotokana na mwendo kasi.

Alisema Wizara yake kwa kushirikiana na ya Ujenzi, itachukua hatua mwafaka ili kuhakikisha ujenzi wa matuta barabarani unafuata viwango.

Alisema ukosefu wa matuta barabarani pia umekuwa ukisababisha uharibifu wa mabasi na hivyo kuongeza gharama za uendeshaji.
Chanzo: Nipashe

Ujumbe wa X-Mass



Zitto Kabwe:Aeleza Kulikoni Yake


Mbunge wa Kigoma kaskazini,
Mheshimiwa Zitto Kabwe

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Zitto Kabwe amesema kuwa hajapewa sumu kama ilivyokuwa imedaiwa huku akisisitiza kuwa hakuna binadamu anayeweza kufanya hivyo.Pia mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini, amesema hana nia wala mpango wa kukihama chama hicho.

Bw. Kabwe aliyasema hayo juzi wakati akiwahutubia mamia ya wananchi Mkoa wa Kigoma katika mkutano wake wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya kawawa ndani ya Manispaa ya Kigoma ujiji.

Alisema kuwa migogoro inayoendelea ndani ya chama chake isiwafanye wananchi wa Kigoma kuwa na hofu yeyote na hata yale yanayoandikwa na vyombo vya habari pia yasiwanyime rah,a waendelee kukisimamia chama chao.

"Wananchi wenzangu msiwe na wasiwasi, mimi ni mzima kabisa, yameandikwa mengi katika vyombo vya habari, mara nimepewa sumu, nataka niwahakikishie hizo habari si za kweli, mimi sijapewa sumu na hakuna binadamu anayeweza kunipa sumu, tuendelee kufanya kazi na kukijenga cha chetu," alisema Kabwe.

Siku za karubuni kumekuwapo na mgogoro ndani ya CHADEMA kutokana na mbunge huyo kutofautiana na wabunge wenzake kuhusu msimamowa kususia hotuba ya Rais jakaya Kikwete bungeni, hali iliyosababisha chama hicho kuundama kamati ya kuzungumza naye kumpa ushauri.hatua hiyo ilichukuliwa siku chache baada ya wabunge wenzake kupiga kura ya kutokuwa na imani naye, kama Naibu Kiongozi wa Kambi ya upinzani bungeni.

Wakati wabunge hao wanachukua uamuzi huo, Bw. Kabwe aliugua ghafla na kulazwa katika Hospitali ya Aga Khan akisumbuliwa na tumbo, na baadhi ya vyombo vya habari vililiripoti kuwa amelishwa sumu, ingawa madaktari walisema ni tumbo lake lilikuwa tu limechafuka.

Katika hatua nyingine Zitto aliitaka Wizara ya Tawala za Mikoa na Serekali za Mitaa (TAMISEMI) kuitisha uchaguzi wa meya wa Kigoma/Ujiji haraka ndani ya wiki mmoja uliokuwa umesimamishwa wiki iliyopita kutokana na mgogoro wa mgawanyo wa madiwani wa viti maalumu.

"Halmashauri zingine tayari zimeshafanya uchaguzi na wamepata meya, na kazi za kuleta maendeleo wameshaanza, sasa wao wanapozidi kutucheleshea sisi kufanya uchaguzi, wajue na kazi ya kuleta maendeleo katika manispaa yetu inazidi kuchelewa," alisema Bw. Kabwe.

Mbunge huyo amewataka viongozi wa vyama mbalimbali nchini kutumia fursa walizozipata katika kuleta maendeleo ya jamii na sio kuendekeza uadui na serikali kuu.
Chanzo: Majira

Friday, December 24, 2010

Ruzuku: CCM milioni 800/-, Chadema 200/-, CUF 117/-


Msajili wa Vyama vya Siasa,John Tendwa
Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, ametangaza viwango vya mgawo wa ruzuku kwa vyama vilivyotimiza sifa, baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, huku kiwango cha mgawo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ilichokuwa ikipata kila mwezi, kikiwa kimeshuka.


Licha ya CCM kuvipita vyama vingine katika viwango vya mgawo uliotangazwa jana na Tendwa, kiwango cha mgawo wake wa ruzuku, kimeshuka kutoka Shilingi bilioni moja ilizokuwa ikipata kila mwezi katika kipindi cha miaka mitano iliyopita kufikia Sh. milioni 800 inazopata hivi sasa.

Kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi, ruzuku hiyo hutolewa kwa chama kilichofikisha kuanzia asilimia tano ya kura za urais na kwa uwiano wa wabunge na madiwani, ambao chama ‘kilivuna’ katika uchaguzi huo.

Mbali na CCM, vyama vingine, ambavyo vinapata ruzuku, baadhi vikilingana na vingine vikitofautiana sifa ya kupata ruzuku hiyo, ni Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi, UDP na TLP. Viwango vya mgawo wa ruzuku hiyo, vilitangazwa na Tendwa alipozungumza na NIPASHE katika mahojiano maalum ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana.

Alisema ruzuku hiyo ilianza kutolewa na ofisi yake kwa vyama hivyo, kuanzia Novemba, baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika nchini Oktoba 31, mwaka huu na ule uliofanyika baadaye katika baadhi ya majimbo kukamilisha uchaguzi huo.

“CCM imeshuka kwa ruzuku. Huko nyuma ilikuwa inapata Shilingi bilioni moja, lakini sasa inapata Sh. milioni 818,” alisema Tendwa.

Hata hivyo, alisema ruzuku kwa uwiano wa madiwani, haijaanza kutolewa kwa vile bado hawajapata takwimu za madiwani, ambao kila chama kilipata, katika uchaguzi huo. “Tunasubiri tuweze kuwa na data za madiwani. Hatuwezi kutoa ruzuku za madiwani bila kupata data. Kwa mfano CCM kuna madiwani wamejiuzulu. Kila mgawo (wa ubunge na madiwani) una fungu lake,” alisema Tendwa. Alisema CCM inapata kiwango hicho, kutokana na kupata asilimia 60.40 ya kura za urais katika uchaguzi huo, ambazo ni sawa na Sh. milioni 354 na asilimia 77 ya wabunge (sawa na Sh. milioni 460) kwa mwezi.

Pia alisema licha ya Chama cha Wananchi (CUF) kupata kura katika majimbo mengi ya uchaguzi, kimepata kiwango kidogo cha mgawo wa ruzuku kulinganisha na Chadema. Alisema hali hiyo inatokana na baadhi ya majimbo kiliyovuna wabunge, kama vile ya kisiwani Pemba kuwa na wapigakura wachache waliokiunga mkono katika uchaguzi huo.

“CUF ilipeleka nguvu kubwa Pemba, lakini huwezi kulinganisha na idadi ya wapigakura kama wa Dar es Salaam,” alisema Tendwa.

Kutokana na hali hiyo, alisema CUF sasa inapata Sh. milioni 117.4, kutokana na kupata asilimia 9.80 ya kura za urais (sawa na Sh. milioni 57.9) na asilimia 10 ya wabunge (sawa na Sh. milioni 56). Alisema katika mgawo huo, Chadema inapata Sh. milioni 203.6, kutokana na kupata asilimia 24 ya kura za urais (sawa na Sh. milioni 146) na asilimia 9.62 ya wabunge (sawa na Sh. milioni milioni 56).

Tendwa alisema vyama vya NCCR-Mageuzi, UDP na TLP havipati ruzuku ya urais kwa vile vilipata chini ya asilimia tano ya kura za urais.

Hata hivyo, alisema NCCR-Mageuzi inapata ruzuku ya Sh. milioni 10, kutokana na kupata asilimia 1.08 ya wabunge wakati UDP na TLP alisema vinapata ruzuku ya Sh. milioni 2.4 kutokana na kupata asilimia 0.42 ya kura za ubunge kila kimoja.

Alisema iwapo viwango vya mgawo wa ruzuku ya madiwani itaongezeka kwa chama husika, viwango hivyo navyo pia vitaongezeka.

Kuhusu fomu za gharama za uchaguzi, ambazo wagombea wanatakiwa kujaza, alisema tarehe ya mwisho, ambayo zinatakiwa ziwe zimerejeshwa ofisini kwake, ni Januari 30, mwakani na kwamba, yeyote atakayekiuka ataadhibiwa kwa mujibu wa sheria. “Wanatakiwa waeleze katika hizo fomu walitumia nini, kiasi gani na kutoka wapi. Wathibitishe kwa risiti,” alisema Tendwa.

Akijibu swali kama kuna mgombea yeyote, ambaye hakujaza fomu, alisema hakuna, isipokuwa aliyekuwa mgombea ubunge kupitia TLP Jimbo la Mtama, mkoani Lindi, Ndaka Wolfugang ndiye aliyechelewa kujaza fomu hiyo.

Kutokana na kasoro hiyo, alisema ofisi yake (Msajili) ilimwekea pingamizi Wolfugang, lakini akarudishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuwania nafasi hiyo kwa maelezo kwamba, kuchelewa kwake kujaza fomu hiyo, kulitokana na kuwekewa pingamizi na aliyekuwa mgombea kupitia CCM, Bernard Membe, ambalo baadaye lilitupwa.
Chanzo: Nipashe

Thursday, December 23, 2010

Christmas Shoes-Nawatakia Maandalizi Mema Ya Krismasi

Nasikitika tukielekea kwenye sherehe ya krismasi wapo watu mikono yao imejaa damu,na kuwa ni wao ndiyo wenye dhamana na haki juu ya maisha ya viumbe wengine.


Hebu Tusahau machungu hayo,kwa kuonyesha kujali kwa umpendae
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...