Tajiri wa klabu ya Chelsea ,Roman Abramovich jitihada zake
za kuwaombea viza vijana wa Kitanzania zimegonga ukuta.
Roman Abramovich,kushoto akiwa na Mpenzi wake
Daria Zukhova,walifanya ziara ya kupanda mlima Kilimanjaro
mwaka jana.
Mwezi septemba mwaka jana,Abramovich na ujumbe wake wa watu 6 ulifanya ziara ya Tanzania kwa ajilii ya kupanda Mlima Kilimanjaro.
Mlima Kilimanjaro wenye urefu wa 19,330ft ndio mlima mrefu kuliko yote Afrika, kwenye kuupanda mlima huo Abramovich alifikia urefu wa 15,100ft nakushindwa kupumua kutokana hali ya hewa kuwa nzito hivyo kupatiwa msaada na Wapagazi nakumuwezesha kufika chini salama.
Kufuatia kitendo cha kiutu cha wapagazi hao,Abramovich aliwaahidi kuwalipa hisani kwa kuwapa mualiko kwenda London kuangalia timu ya Chelsea itakapokuwa uwanjani kwenye ligi kuu ya Uingereza.
Lakini jitihada zake hazikufanikiwa kufuatia Ubalozi wa Uingereza kuwakatalia vijana hao Viza mara mbili kwa shaka ya kutoroka pindi watakapo kuwa nchini Uingereza.
Licha ya timu ya Chelsea kutoa mualiko na kutayarisha mazingira ya ujio wao kwa kuandaa usafiri wa kwenda na kurudi,malazi na vyakula,juhudi zote hazikuweza kubadilisha msimamo wa Ubalozi wa Uingereza nchini Tanzania kubadili msimamo wake.
Chanzo: Telegraph
Wakati huo huo Chelsea imepokwa ushindi Dakika ya lala salama
Na matokeo ya kawa Chelsea 3 Vs Aston Villa 3
No comments:
Post a Comment