Mtazamohalisi

Saturday, November 13, 2010

Kesi ya Ghailani yaendelea kusikilizwa mjini New York

Wakili wa Ghailani azisuta hoja za upande wa mashtaka na kuhoji mteja wake hakuwa akijua chochote kuhusu mashambulio ya kigaidi ya mwaka 1998
Ahmed Khalfan Ghailani akiwa mahakamani

Mawakili wa Mtanzania Ahmed Khalfan Ghailani, anaetuhumiwa kushiriki katika mashambulio dhidi ya balozi za Marekani nchini Tanzania na Kenya mnamo mwaka 1998 wanahoji mtuhumiwa huyo hana hatia.
Mnamo siku ya pili ya kusikilizwa hoja za mwisho mwisho katika kesi hiyo, iliyoanza kusikilizwa October 12 mwaka huu,wakili Peter Quijano amehakikisha kwamba mteja wake "hakuwa akijua chochote na kwamba alidanganywa."
Wakili huyo amekosoa pia ushahidi uliotolewa na serikali, akisema "ni dhaifu na wa kutiliwa shaka."
Amekanusha pia hoja kwamba Ghailani alikwenda Pakistan kabla ya mashambulio hayo kutokea.
"Ingekua Ahmed alikuwa ndani ya ndege iliyokuwa ikielekea Pakistan, mngemsikia japo shahidi mmoja. Hakujakuwa na hata mmoja. Ahmed hajakuwemo ndani ya ndege hiyo na nyaraka zilizotolewa ni za bandia." Ameshadidia wakili Peter Quijano.
Mashambulio ya Agosti saba mwaka 1998 dhidi ya ofisi za ubalozi wa Marekani nchini Tanzania na Kenya yaligharimu maisha ya watu 224 na zaidi ya 5000 kujeruhiwa.
Mwenyewe mtuhumiwa, Ahmed Khalfan Ghailani, mwenye umri wa miaka 36 hivi sasa, alikuwepo katika ukumbi wa mahakama akivalia shati rangi ya buluu na tai ya rangi hiyo hiyo.
Anatupiwa lawama ya kuhusika na visa 286 vya uhalifu, ikiwa ni pamoja na "njama ya kutaka kuwauwa Wamarekani."
Wakili wa upande wa mashtaka, Michael Farbiarz, anasema "hoja hizo hazina msingi." Anasema:" Siku ya mashambulio, Ahmed Ghailani aliacha kila kitu alichokuwa nacho maishani mwake, marafiki zake, familia yake, kazi yake na jina lake. Ghailani ni muongo, hakuna maana kwa hivyo kudai amedanganywa."
Wadadisi wanajiuliza kama kisheria ni sawa kesi hiyo kusikilizwa nchini Marekani katika wakati ambapo mashambulio yametokea Afrika mashariki.
Baada ya kusikilizwa hoja za pande zote mbili, na jaji Lewis Kaplan kutoa neno lake, jopo la majaji litaanza kushauriana hii leo.

Mjue Lucas Radebe


Lucas Radebe





 Na Rashid Seif:
katika lugha ya kiswahili unasoma kama lucas Ghadebe,
lucas radebe amekulia katika familia ya watoto 11 katika maisha magumu ya moja ya sehemu zilizokuwa na machafuko makubwa ya kisiasa za ubaguzi wa rangi huko soweto(south western townships).hii ilimpelekea kuja kuwa mmoja katika wachezaji walioheshimika katika ligi kuu ya uingereza na kuwa muafrika kusini wa kwanza kucheza mechi nyingi kuliko wote kwenye timu ya taifa bafana bafana akiwa ameichezea mara 70.
Radebe alinyanyukia kuwa mchezaji muhimu na maarufu mara baada ya kuchaguliwa kuwa nahodha wa timu ya leeds united mwaka 1998.akichukuwa jukumu la kuiongoza timu yenye vijana na wachezaji wengine wenye uzoefu wa ligi kuu.
chini ya uongozi wake radebe leeds united kutoka yorkshire ilinyanyukia kuwa moja ya timu kali katika ligi ya uingereza .Radebe mchango wake haukuwa tu katika uongozi wake bali pia usakataji wake safi wa kandanda usio na utata dhidi ya washambuliaji wa timu pinzani ambao ulimfanya aheshimike duniani na wanasoka wenzake.
HAPO MWANZONI
alikulia katika ukanda wa 4 wa mji wa DIEPKLOOF katika kitongoji cha soweto nje ya jiji la johannesburg.Radebe akishuhudia machafuko ya kisiasa akiwa na umri wa miaka 15 wazazi wake walimpeleka akaishi katika mji wa BOPHUTHASWANA ambao ni mmoja kati ya miji iliyotengwa kwa ajili ya watu weusi katika kipindi cha siasa za ubaguzi wa rangi.alianza kucheza mpira kama sehemu ya kujishughulisha akianza kama mlinda mlango kabla hajabadili kuchezea nafasi ya kiungo na kujiunga na timu ya ICL iliyokuwa ikichezea ligi iliyojulikana kama ligi ya boputhaswana .
mwaka 1989 kipaji chake kilgundulika na timu na moja ya timu kongwe barani afrika ijulikanayo kama kaizer chiefs ambayo alitia mkataba nayo.wakimtaka achezee kama mlinzi wa kati badala ya kiungo....inaendelea

Daw Aung San Suu Kyi (Mother of True Burma), released



The Burmese military authorities have released the pro-democracy leader, Aung San Suu Kyi, from house arrest.
Appearing outside her home in Rangoon, Ms Suu Kyi told thousands of jubilant supporters they had to "work in unison" to achieve their goals.It is not yet clear if any conditions have been placed on her release.

Like the South African leader Nelson Mandela, Aung San Suu Kyi has become an international symbol of heroic and peaceful resistance in the face of oppression. For the Burmese people, Ms Suu Kyi, 64, represents their best and perhaps sole hope that one day there will be an end to the country's military repression. As a pro-democracy campaigner and leader of the opposition National League for Democracy party (NLD),she has spent more than 11 of the past 19 years in some form of detention under Burma's military regime In 1991 she was awarded the Nobel Peace Prize for her efforts to bring democracy to Burma. At the presentation, the Chairman of the Nobel Peace Prize Committee, Francis Sejested, called her "an outstanding example of the power.

For more about  her, listen her documentary of " freedom from fear".
http://www.bbc.co.uk/iplayer/episode/b00sq2n1/Freedom_from_Fear_Aung_San_Suu_Kyi

Haile Gebrselassie Atangaza Kustaafu Mbio

Haile Gebrselassie
                                                                                                                                                              
Usain Bolt akiwa na Haile Gebrselassie
Haile Gebrselassie ,nguli wa mbio ndefu duniani atangaza kustaafu, kwa kushindwa kumalizia mbio na kuishia umbali  wa maili 16 baada ya maumivu ya kuwa na maji kwenye goti la kulia. Alikuwa akishiriki mbio za nyika za jiji la Newyork.

Amesema "hakufikiria kustaafu" "lakini kwa mara ya kwanza leo hii imebidi.Imefika wakati wa kuangalia shuguli nyengine".Aliongezea kwa kusema" Nimeona wana michezo wengi wakipanga muda wa kustaafu. Anasema  haiwi hivyo. Siku ambayo umetangaza kustaafu, basi ndiyo tayari umestaafu kwenye akili yako".

Haile Gebrselassie ameweza kuvunja rekodi za dunia 27, zikiwamo mbio za nyika za mita 5000 na mita 10000. Ameshinda medali ya dhahabu mwaka 1996 katika mbio za mita 10000 huko Atlanta na mwaka 2000 Sydney Olympics.

Bingwa wa dunia katika mbio za mita 10000 toka 1993- 1999, kwa muda wa miaka minne mfululizo.
Ni mkimbiaji mwenye kasi kwa umbali wowote  kwenye kumbukumbu za mbio, toka dakika 3:31.76 sekunde kwenye umbali wa mita 1500 hadi masaa 2 na dakika 3 na sekunde 59 kwa mbio za nyika. Mwaka 1999 hadi 2000 hajawahi kushindwa katika mbio zozote alizoshiriki kwa muda wa miaka 2 mfululizo.

Hakika, utakumbukwa kwa kuliletea bara la Afrika heshima. Uzoefu unaonesha, itachukua muda kupata mrithi wako. Hata Tanzania , hadi leo hii hawajapata wanariadha walioliletea Taifa heshima kama Filbert Bayi na Juma Ikangaa.

Friday, November 12, 2010

Malikia Elizabeth ajiunga na facebook, na kukutana na kashfa

Malikia Elizabeth wa Uingereza
Hivi karibuni, Queens Elizabeth II alijiunga na facebook na siku moja baada ya kujiunga katika tovuti hii ya jamii ukurasa wake ulijaa maoni machafu kutoka kwa watu . Walengwa wakuu walikuwa Carmilla na Charles na picha zao zilishambuliwa kwa maoni ya matusi.
Ukurasa  huu wa Familia ya Kifalme ya Uingereza, ulizinduliwa Novemba 8 pamoja na akaunti ya Twitter na Flickr. Wakati watu zaidi ya 220,000 "waliipenda", picha 28 katika albamu zilishambuliwa kwa maoni ya aibu na matusi.Familia ya kifalme ina wafuasi zaidi ya 75,500 kwenye Twitter na huweka picha mpya katika akaunti yake  ya Flickr kila siku. Pia ina channel kwenye Youtube

Saudi Arabia yaimarisha ulinzi Mecca

Mecca-Saudi Arabia

Kiasi ya mahujaji wa Kiislamu millioni mbili na nusu wanaanza kumiminika katika mji wa mtakatifu wa Makkah, huko Saudi Arabia, huku ulinzi ukiimarishwa kwenye mji huo ambao umewekwa vifaa vipya vya kisasa, ukiwemo usafiri wa treni kurahisisha zoezi hilo la Hijja.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Saudi Arabia, mwanamfalme Nayef bin Abdul Aziz, amesema hawawezi kulipuuza tishio la kundi la kigaidi la Al-Qaida kushambulia wakati wa Hijja hiyo ya siku tano inayoanza kesho kutwa, Jumapili, ijapokuwa kundi hilo halijawahi kufanya shambulio lolote dhidi ya hijja hapo kabla.
Hapo siku ya Jumatano, waziri huyo wa ndani wa Saudi Arabia alielezea kitisho cha  kundi la Al-Qaida kushambulia, lakini hata hivyo akasema uwezekano ni mdogo wa kufanya hivyo.

Dar-es- Salaam, Tanzania
MAHUJAJI 20 waliokuwa wasafiri kwa ndege ya Shirika la Eggypt na Ethiopia kwenda Hijja Meccah na Madina wamekwama uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere wa Dar es Salaam baada ya kutapeliwa fedha zao. Abiria hao ambao walieleza kuwa walipanga safari hiyo kupitia taasisi ya Taibah ya jijini Dar es Salaam, wamekwama kuondoka baada ya taasisi hiyo kuwakana.
Baadhi ya abiria hao waliozungumza na Mwananchi katika ofisi za Taibah jana walisema walilalamikia kitendo hicho na kukiita cha kikatili kwa kuwa hata fedha zao hawajalipwa. Salma Abedi alisema alilipa Sh5.5 milioni kwa ajili ya safari hiyo kwenda na kurudi, chakula na malazi kwa juma moja.

“Kwa kifupi la kusema sina kwani nikikumbuka jinsi nilivyohangaika kuipata hii safari sitaki kuamini eti leo naambiwa hakuna safari wakati Paspoti ninayo na nilikuwa katika listi ya watu wanaoondoka,”alisema Abedi. “Leo hadi muda huu hawajafungua ofisi inavyoonekana haitofunguliwa hebu niambie huu si utapeli huu.

“Nimetoa dola elfu tatu na mia moja kugharamikia safari hii,nimetokea Kongo na nimelipia katika shirika hili nikitegemea kuondoka na ndege iliyoondoka tangu juzi, lakini cha ajabu nimeambiwa safari hakuna na viongozi siwaoni,”alisema Abdalah Abeidi ambaye ni raia wa Kongo.

“Hapa unaponiona nimekuja tangu Oktoba 25, mwaka huu, nimefikia hotelini ambako mpaka leo hii muda wangu wa kukaa pale umekwisha na sina tena fedha za kulipia na mimi hapa ni mgeni sina ndugu nitaenda wapi?sina la zaidi ninachotaka nipewe fedha zangu tu,”alisema Abeidi. Mwenyekiti wa NGO Mkoa wa Tanga Saida Sharifu ambaye nae ni mmoja wa mahujaji alisema amesikitishwa na kitendo cha Taasisi hiyo kwa kudhulumu haki yake.

“Mimi nilitoka Tanga kwa madhumuni ya kwenda katika Hijja na nililipia fedha katika taasisi hii ya Taibah,kitendo cha wao kukimbia ni kitendo kibaya na kinachoumiza kwani kuna watu walifika hadi uwanja wa ndege ila wakarudishwa wengine hawana fedha, kifupi tumedhalilishwa sana,”alisema Sharifu. Aliiomba serikali kufuatilia taasisi hiyo na kuichukulia hatua kwani ni aibu kubwa kwa taasisi ya dini kufanya jambo kama hilo.


Safari hiyo ya kwenda kuhiji Makka na Madina ilikuwa inagharimu Sh 55 milioni ambayo inajumuisha malazi,chakula na usafiri wa kwenda na kurudi. Mbali na hayo, taasisi hiyo ilitoa hati feki ya kusafiria kwa watu na kusababisha mtu mmoja kuwekwa rumande katika uwanja wa ndege wa kimataifa kwa kukutwa na hati hiyo.

Mweka hazina wa taasisi ya Taibah iliyoandaa safari hiyo, Ali Momba alisema taasisi hiyo haiwatambui mahujaji hao kwa kuwa walilipa fedha zao nje ya ofisi. "Hawa walilipa fedha nje ya ofisi zetu na sisi hatuna majina yao," alisema Momba.
  
Ningependa kuwapa pole kwa usumbufu mahujaji waliopatwa na kadhia hii, na kutoa wito kwa serikali kuchukua hatua muafaka za kudhibiti makampuni ya uwakala wa hijja ili aibu kama hii isijirudie.
Hii si mara ya kwanza kwa mahujaji kujikuta katika usumbufu kama huu ,mwaka 2007 ili wachukua zaidi ya wiki na kuilazimu serikali kuingilia kati .

Spika wa Zamani Mh.Samuel Sitta akila kiapo cha Ubunge

Spika Mstaafu Samuel Sitta


Mheshimiwa Samuel Sitta ,Mbunge wa Urambo Mashariki akila kiapo cha Mbunge mbele ya Naibu wake wa zamani na mrithi wake wa kiti cha Uspika Bi.Anna Makinda.

Hongera kwa kuonesha ukomavu, Mheshimiwa Sitta sauti yako dhidi ya ufisadi kwa Taifa letu tungali tukiihitaji.Kwa kuwa mchezo wa siasa  ni kitendawili ikiwa utateuliwa kuwa waziri bado tunakuomba uendelee kuwa mpiganaji hadi pumzi yako ya mwisho.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...