Mtazamohalisi

Saturday, October 16, 2010

Yasijirudie Ya Uchaguzi Mkuu 2010 kwenye Uchaguzi Mkuu 2015

Rais Jakaya M.Kikwete

viongozi wa vyama vya siasa nchi

Kukataa mdahalo
Napinga kitendo cha CCM kukataa midahalo kwa madai wananchi wanajua mazuri waliyofanya na watakayofanya.
Hii haikubaliki kwani bado umewanyima wananchi fursa nzuri ya "kuchambua mchele na chuya".

Vyama kuwasahau wapiga kura
Hii mara nyingi inatokea baada ya uchaguzi, vyama vinaacha kukita mizizi katika maeneo walikoshinda au kushindwa. Kufanya hivyo hakuleti picha nzuri kwa wananchi, kwani wao huonekana muhimu tu wakati wa kuomba kura.

Vyama kutokuwa na mipango ya muda mrefu
Mbali na CCM inajulikana na kila mtu kuwa Rais Jakaya Kikwete anamaliza muda wake,hivyo kuna harakati za kumtafuta mrithi wake.
Na kwa utaratibu wa CCM chama hakina mtu ila kina wenyewe nakwa mtindo huo ,mfumo wa uongozi upo wazi hivyo chama hakimtegemei mtu ila kinajitegemea kutokana na mfumo wake.
Kuhusu vyama vya siasa hilo nalo muhimu kulitambua, chama si mali ya mtu bali chama kinabakia kuwa ni wanachama hivyo basi wajenge misingi mizuri yakuachiana madaraka.Kuhusu mipango mengine vyama lazima viweke misingi imara ya kuingia katika serikali za mitaa kabla uchaguzi mkuu hii itasaidia kujua jinsi gani wanakubalika ili wafanye marekebisho yakisera yatakayoweza kuwashawishi wapiga kura.

Ahadi kwa watu wenye kuhitaji msaada maalum
Tumeona vyama katika nyingi ya ahadi zao wamesahau kuwa watu wenye kuhitaji msaada maalum kama viziwi,vipofu,wazee na maalbino kuwa ni muhimu katika jamii.Kwa mfano hakuna chama kilichosema nitasaidia kufungua shule au kuboresha zilizopo kwa watu wajamii hii,tumeona pia kuna uwindwaji kama wanyama kwa wazee na maalbino.Je! hili la usalama wao halizungumziki? maana haifai baadae kutaka umaarufu kupitia jamii hii.

Katika serikali za awamu zote nne zimejikita zaidi katika masuala ya miundo mbinu pamoja na maji,tunaomba mwaka 2015 iwe ahadi hizi kuwa ni basi maana nijukumu la Serikali kulitekeleza hilo nasio mambo yakutaka kudai kura.Muhimu kwa kila mgombea kuja na nini? atafanya kuondoa tatizo la ajira na mipango ya kupunguza umaskini,ujinga na maradhi.
Itaendelea sehemu ya pili..................

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...